Malengo yetu

JITA VOCATIONAL TRAINING CENTRE ina malengo yafuatayo:


  • Kutoa elimu ya ujuzi kwa watu wote hasa wale waliokata tamaa kwa kudhani kufeli mtihani ndio kufeli maisha.
  • Kushirikiana na wadau mbali mbali katika kuhakikisha tunawafikia vijana wengi Tanzania ili kupunguza tatizo la ajira nchini.
  • Kushirikiana na serikali katika kupunguza vijana wanaozagaa mtaani kwa kukosa shughuli maalum ya kufanya.
  • Kutoa elimu ya kujitambua kwa vijana ili wawe nguzo ya kuijenga Tanzania
  • Kupunguza vitendo viovu katika jamii hasa uvutaji bangi, madawa ya kulevya, ubakaji kwa kuwapatia vijana elimu ya ujuzi itakayowasaidia kuwa na kazi badala ya kujikita katika shughuli na matendo maovu.
  • kuwapa moyo wale wote waliokata tamaa kwa kuwaonesha njia mbadala ya kuishi na kuyafurahia maisha yao kama wengine.

No comments:

Post a Comment